Viongozi wa mataifa wanachama wa kundi la G20
wanakusanyika katika mji wa St Petersburg nchini Urusi kwa mkutano wao wa kila
mwaka wa mataifa ishirini yenye ustawi mkubwa wa kiviwanda duniani.
Duru zinasema maswala
ya kiuchumi huenda yakafumbiwa macho katika mkutano huo kutokana na mzozo
uliopo nchini Syria na tofauti zilizopo kati ya Marekani na Urusi kuhusu
mipango ya kuishambulia Syria kwa madai ya kutumia silaha za kemikali.
Rais Barack Obama
anasema kuwa dunia haiwezi kuepuka tendo la kutochukua hatua dhidi ya Serikali
ya Syria.
Naye Rais Vladimir
Putin amesema kuwa Marekani ikishambulia Syria litakuwa tendo la uchokozi. Rais
wa Marekani ameeleza kwamba Serikali ya Syria imekaidi marufuku ya kimataifa ya
kutumia silaha za kemikali na hatua inapaswa kuchukuliwa.
Kiongozi wa Urusi anasema
vingine kuwa Marekani kushambulia Syria bila idhini ya Umoja wa Mataifa ni
kukiuka sheria ya kimataifa.
Hapa hali ya maoni
mawili yanayohitiliafiana kutoka kwa Marais wawili maarufu.
Inaonekana kuwa
tofauti kubwa inayohusu Syria huenda ikapata nafasi bora katika vyombo vya
habari kuliko mkutano unaoendelea wa mataifa tajiri zaidi duniani ya G20.
Marais hawa wawili ni wanachama wa G20 ambapo watataka kushawishi mataifa
kuunga mkono upande wao.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment