Kenya inaanza siku tatu za maombolezi
ya kitaifa kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika jengo
la kibiashara la Westgate mjini Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta pia ameseama kuwa bendera zitapepershwa nusu
mlingoti kwa heshima ya waliopoteza maisha yao katika mashambulizi hayo.
Watu 67 wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa wa usalama, ingawa
kuna hofu kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa uchunguzi wa kimataifa wanaungana na wale wa Kenya
kujaribu kuondoa mili ambayo imenaswa kwenye vifusi vya jengo hilo ambalo sehemu
yake iliporomoka jana. Nia ni kujaribu pia kutambua uraia wa washambulizi hao.
Baraza la usalama wa kitaifa linatarajiwa kukutana leo kudadisi
yaliyotokea na kujiandaa kwa mkakati mpya wa kigaidi.
Magaidi watato wa kundi la Al Shabaa lililokiri kutekeleza
mashambulizi hayo,waliuawa katika shambulizi hilo lililodumu siku nne na kuwa
washukiwa wengine 11 walikamatwa wakijaribu kuondoka nchini.
Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumatano , Rais Uhuru
Kenyatta alisema kuwa alihisi uchungu mkubwa na kuwa Kenya imejeruhiwa
vibaya,lakini alielezea matumaini kwa kuwa shambulizi limeisha na kusema kwamba
waliohusika watakiona cha mtemakuni.
Wakati huohuo, afisaa mmoja mkuu wa serikali ya Somalia, amesema
kuwa hakuna suluhu la kijeshi kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabaab nchini
humo. Wanamgambo hao wameitikia kuhusika na mashambulizi ya kigaidi nchini
Kenya ambao watu zaidi ya sitini wameuawa.
Akizungumza na mjumbe wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa,
Yusuf Mohamed Ismail Bari Bari, alisema kuwa serikali yake na jamii ya
kimataifa inapaswa, kungazia zaidi mizizi ya tatizo la magaidi hao, upatikanaji
wa rasilimali pamoja na uwakilishi wa kisiasa.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment