Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanajiandaa kurejea
nchini Syria kuendelea na uchunguzi kuhusu ikiwa silaha za kemikali zilitumika
katika miji mingine ya nchi hiyo mbali na Damascus
Wachunguzi
hao tayari wamethibitisha kuwa gesi ya sumu aina ya Sarin, ilitumika katika
kuwashambulia watu katika kitongoji kimoja cha Damascus mwezi Agosti tarehe 21
ambapo mamia waliuawa.
Sasa
wanajiandaa kutembelea maeneo mengine matatu ambako inaaminika silaha za sumu
zilitumika ingawa kwa kiwango kidogo mapema mwaka huu. Shambulizi lilifanyika
katika eneo la Aleppo,mjini Homs na karibu na Damascus.
Serikali
ya Syria pamoja na waasi zinatuhumiana kwa kufanya mashambulizi .Wachunguzi hao
wataamua ikiwa silaha za kemikali zilitumika lakini hawatasema ni nani wa
kulaumiwa
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment