Polisi nchini Sudan wamewatifulia gesi ya kutoa
machozi waandamanaji katika Mji Mkuu Khartoum, huku wengi wakiendelea
kukasirishwa na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta.
Walioshuhudia maandamano hayo walisema kuwa
waandamanaji waliteketeza jengo moja la Chuo Kikuu na vituo kadhaa vya petroli.
Pia waliziba njia kuu ya kuelekea uwanja wa ndege.
Watu wawili wameuawa tangu maandamano hayo
kuanza Jumatatu wakati Serikali ilipotangaza kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta.
Hatua hiyo imefikiwa katika juhudi za
serikali kuongeza mapato ya Serikali.
Hata hivyo waandishi wa habari hapo mjini
wanasema kuwa hatua hiyo imewaathiri zaidi watu wa mapato ya chini na kuzusha
Serikali kuchukiwa na raia wa kawaida.
Duru zinasema kuwa watu watatu wamefariki
kutokana na ghasia hizo. Waziri wa elimu naye amesema kuwa shule ziliko katika
mji mkuu zitasalia kufungwa hadi Septemba tarehe 30.
Kwa mujibu wa shirika la AFP, watumijai wa
mtandao wa internet wanasema kuwa huduma zimekatizwa ingawa haijulikani ikiwa
ni hatua ya serikali kudhibiti mawasiliano au ilitokana na hitilafu za
kimitambo.
Serikali ilitangaza Jumatatu hatua zaidi za
kupandisha bei ya mafuta baada ya kusitisha ruzuku kwa muda katika juhudi za
kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini humo.
Mnamo siku ya Jumanne waandamanaji
waliteketeza ofisi za chama tawala,mjini Omdurman.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment