Wakuu wa idara ya Polisi nchini Kenya
wamewaonya waandisi wa habari kuhusu walivyoripoti matukio katika jumba la
Westgate ambako magaidi walishambulia zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Onyo hili linakuja baada ya taarifa za wanajeshi kufanya uporaji
katika jengo hilo wakati wakipambana na magaidi hao waliokuwa wamewateka nyara
watu waliokuweme ndani ya jumba hilo.
Mkuu wa polisi, David Kimaiyo alisema kuwa waandishi hawapaswi
kutoa kuchochea Propaganda, au kuwachochea wakenya wakati wakipeperusha
matangazo yao.
Duru zinasema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamehojiwa na
polisi hii leo.
Picha za CCTV zilizofichuliwa kwa waandishi wa habari
zilionyesha wanajeshi wakitoka ndani ya jumba hilo na mifuko ya plastiki
zilizoshukiwa kuwa na bidhaa kutoka katika mojawapo ya maduka makubwa
yaliyokuwa ndani ya jengo hilo la Nakumatt.
Hata hivyo jeshi limekanusha madai hayo na kusema kuwa wanajeshi
walikuwa wanachukua maji ya kunywa wakati wa operesheni yao dhidi ya magaidi.
Takriban watu 67 walifariki ikiwemo wanajeshi na mamia ya
wengine kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo liliosababishwa na Al Shabaab kama
walivyokiri. Waliwateka nyara watu ndani ya jingo hilo kwa siku nne.
Pamoja na kupora, vyomo vya habari Kenya vimesema kuwa baadhi ya
wanajeshi waliuwana na wenzao wakati wa operesheni yao kutoka na kile
kilichosemekana kuwa ukosefu wa maelekezo mazuri kuoka kwa wakuu wa usalama.
Kutoka
BBC.
0 maoni:
Post a Comment