Mtu mmoja anahofiwa kuuwawa na wengine
kadhaa kujeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi kati ya polisi na watu
waliobeba silaha hatari ambao wamewateka nyara wateja ndani ya jengo lenya
maduka duka la Westgate Shopping Mall katika mtaa wa Westlands, Nairobi.
Hadi
sasa hakuna maelezo yoyote kuhusu lengo la washambuliaji hao ingawa taarifa za
Polisi zinanazungumzia uwezekano kua ni shambulio la kigadi.
Mkuu
wa polisi David Kimaiyo anaongoza juhudi za kuwaokoa mateka wanaozuliwa ndani
ya jengo hilo..
Kimaiyo
akitumia mtandao wa twitter anasema jengo hilo limezingirwa na polisi . Na
polisi wameweza kudhibiti sehemu ya chini ya jengo. Na amewataka watu
wsilisogelee eneo hilo.
0 maoni:
Post a Comment