Watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye
eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya
yalitumika.
Inaarifiwa watu watano wamekufa.
Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji
inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama
wapiganaji hao wamehusika.
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka
liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu
waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.
Inaarifiwa kuwa watu wengi wamenasa ndani ya jengo.
Magari yaliyoegeshwa nje ya maduka yameharibika
0 maoni:
Post a Comment