Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na
magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate
Katika ukurasa huu tutakupasha moja kwa moja matukio yanavyojiri
katika jengo la Westgate.
Ikiwa uko karibu na jengo hilo unaweza kutupasha hali unavyoiona
kupitia kwa ukurasa wetu wa Bofyafacebook
bbcswahili
BofyaFacebook:Halima
Msuya kutoka Moshi kupitia BofyabbcswahiliAmeandika
Poleni sana ndugu zetu Mungu yu pamoja nanyi.
BofyaFacebook:Mohamed
Kahogo Wa Morogorogo Tzn asema kwenye ukrasa wa BofyabbcswahiliEee
Mola wajaalie hawa ndugu zetu wakenya!waushide mtihani huu AMEEEN.
15:33 Waziri wa usalama wa Kenya Joseph Ole Lenku asema kuwa
wanajeshi wameweza kudhibiti jengo lote la Westgate
15:20 Polisi waonekana wakikimbia huku na kule katika harakati
zao hizo dhidi ya Al Shabaab
Juhudi za uokozi Westgate
14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema
magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi
litakabiliana nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa
kimataifa
14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya
usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao...Hadi kufika sasa watu
62 wamefariki na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa. Pia ameongeza kuwa magaiodi
wote ni wanaume, kutokana na taarifa za awali kuwa magaidi hao walikuwa
wanaongozwa na mwanamke
14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na
wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia
amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili
14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi
ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya jengo hilo
kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao
Moshi mkubwa ukitoka ndani ya jumba la Westgate
14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama
vinakaribia kudhibiti jengo hilo lote na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo
kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka
14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo
13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika eneo la
Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa
ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo
13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la
shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu
kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao
Waathiriwa wa shambulizi la Westgate
13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu
katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha
13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la
Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao
idadi yao haijulikani
13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al
Shabaab
12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika
jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment