Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba nchini Tanzania
Joseph Kanik, na Bondia mkali Tanzania, Mkwanda Matumla, wamekamatwa na madawa
ya kulevya huko mjini Addis Ababa, nchini Ehtiopia.
Wawili hao walikamatwa mnamo Agosti 31, mwaka huu
katika kiwanja cha ndenge mjini Addis Ababa, walipokuwa wakisubili Ndege ya
kwenda nchini Ufaransa, zile pande za bata nyingi Paris, bado wapo
wanashikiliwa na Polisi wa kitengo cha makosa ya jinai nchini Humo, hayo
yalitolewa na Balozi wa Tanzania.
Kutokana na sheria za nchi hiyo wakikutwa na hatia
wanaweza kufungwa kifungo cha miaka 9 hadi 15, inasemekana kuwa wanamichezo hao
watafungwa uko uko kutokana na kuwa nchi hizi mbili hazikuwa na utaratibu wa
kubadilishana wafungwa, kutokana na jambo hilo kuna kila dalili za wachezaji
hao kutumikia kifungo nchini Ehtiopia.
“
wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10, sisi tulipigiwa simu na
polisi wa hapa Alhamisi iliyopita kujulishwa kwamba kuna watanzania wawili
wameshikiriwa kwa tuhuma za kukutwa na Dawa za kulvya (SUMU)tulipokwenda
tukamkuta ni Kaniki, na Matumla, yalikuwa maneno ya Balozi huyo wa Tanzania nchini
Ethiopia,.”
Kaniki alijitetea kuwa Mzigo haukuwa wake bali
ulikuwa wa Mkwanda, ndiye anayemjua vizuri mwenye mzigo huo, yeye alimsaidia tu
kwa kuwa walikuwa katika safari moja na inasemekana kuwa mzigo huo ulichukuliwa
nchini Kenya, Mombasa, na walipofika tu Addis Ababa, mkwanda alifanikiwa
kupenya hadi kwenye ndege lakini Kaniki, alikamatwa na Mbwa wa kunusa madawa ya
kulevya, lakini alikana na kusema mzigo ni wa matumla.
0 maoni:
Post a Comment