Rais wa Marekani Barack Obama, amesema kuwa
atafanya juhudi zaidi za kidiplomasia kuangamiza zana za kemikali za Syria ,
lakini pia ameambia jeshi lake kuwa tayari kuchukua hatua ikiwa juhudi zake
zitafeli.
Kwenye hotuba yake ,
Obama alisema kuwa amelitaka baraza la Congress kuakhirisha kura yake kuhusu
kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Syria.
Marekani imetishia
kufanya mashambulizi ya angani baada ya shambulizi la kemikali kuwaua mamia ya
watu mjini Damascus mwezi jana.
Urusi imependekeza
kuwa silaha hizi ziwekwe chini ya udhibiti wa jamii ya kimataifa.
Ingawa maafisa wa
Syria wamekubali kutii agizo la Marekani, nchi hiyo pamoja na washirika wake
wana wasiwasi ikiwa Syria itafanya kama inavyosema.
Athari za vita nchini
Syria , watoto hawajasazwa
Mpango wa Urusi
ulisababisha siku moja ya mashauriano mazito ya kidiplomasia katika Umoja wa
Mataifa siku ya Jumanne.
Akiongea katika Ikulu
ya White House, Obama alisema kuwa serikali yake, ilikataa wito wa kuchukua
hatua za kijeshi dhidi ya Syria kwa sababu haamini ikiwa kutumia nguvu
itasuluhisha mgogoro huo.
Lakini alisema kuwa
alibadili msimamo wake baada ya zana za kemikali kutumiwa kwenye mashambulizi
katika viunga vya mji wa Damascus tarehe 21 mwezi Agosti.
"usiku huo, dunia
nzima iliona kwa kina athari mbaya za zana za kemikali na kwa nini watu wengi
duniani wanahisi kuwa zana hizo hazipaswi kabisa kutumiwa, ni uhalifu dhidi ya
binadamu na ukiukwaji wa sheria za vita,'' alisema Obama.
Serikali ya Syria
imekanusha kuwa ilitumia silaha za kemikali kushambulia watu na badala yake
imelaumu waasi ikisema walizitumia katika juhudi zao za kutaka kumng'oa
mamlakani Rais Bashar al-Assad
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment