Serikali ya Kenya imetangaza ugunduzi wa visima
vikubwa vya maji chini ya ardhi ambavyo vinaweza kumudu mahitaji ya maji katika
kipindi cha zaidi ya miaka hamsini ijayo katika jimbo la Turkana na kwa nchi
nzima.
Visima hivyo bila
shaka vitaleta afueni kwa wakaazi kwani Turkana ni eneo kame Kaskazini
Magharibi mwa Kenya. Eneo hilo pia lina viwango vya juu vya umaskini.
Ugunduzi huo ulitokana
na utafiti wa wanasayansi waliotumia teknolojia ya satellite
Visima hivyo vinapata
maji kutoka kwa chemichemi za maji kutoka milima ya mbali kwa hivyo maji yake
yakitumiwa vyema huenda havitawahi kukauka.
Mamilioni ya wakenya
wanakosa maji safi.
Nchi hiyo pia
inakabiliwa na msimu tata wa mvua na inakabiliwa na athari za mabadiliko ya
tabia nchi.
Utafiti ulifanywa na
shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO na wanasayansi wa Kenya kwa ufadhili wa
serikali ya Japan.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment