Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya
MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa
magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya
kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani
na mshikamano ulipo nchini.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa
siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba
333 la tarehe 27 septemba,2013.
Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.
Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.
Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17
Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA
ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwe na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.
Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la
Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.
Jambo ambalo halikuwa la ukweli.
.Jeshi la Polisi
katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti. Serikali na
jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa
hiyo Jeshi lake hakiwezi kupitisaha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari
iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi
na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya
ibada.
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa
siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye
uchochezi.
Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo
wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za
fani ya Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha
kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20
Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12
Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013
katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari
kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo
unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu
mithili ya damu nyingi kumwagika.
Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila
uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu
wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa
goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina
lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione
kuwa haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia
gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government
Notice No.332) la tarehe 27 Septemba, 2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri
kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia
taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.
Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia
uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya
kuvifungia. Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha
uvunjifu wa amani nchini.
Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013
0 maoni:
Post a Comment