Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi, waziri wa mambo ya
ndani ya nchi wa Kenya alitupilia mbali swala kwamba serikali ya Kenya ingefaa
kuzindukana baada ya kupata habari mapema kwamba kuna uwezekano wa shambulio
kubwa la kigaidi kutokea katika mji mkuu.
Waziri Joseph Ole Lenku alilitoa maanani swala hilo la mwandishi
wa BBC na kusema kuwa taarifa za ujasusi, yaani intelijensi, ni swala la
serikali:
"Sifikiri kama weye ndie wa kuniambia mimi nini serikali
ingefaa kusema au la.
Kuhusu taarifa na ujasusi wetu, hilo halijakuhusu.
Tumeonesha hapa, na tunaendelea kusema, kuwa taarifa za ujasusi
zitabaki hivohivo, habari za ujasusi; na hatutasema hadharani.
Kwa hivo intelijensia yetu ni siri na siyo kitu tutakizungumza
hadharani."
Waziri huyo wa Kenya piya alizilaumu nchi, pamoja na Marekani,
ambazo zimeonya wananchi wao wasiende Kenya.
Alisema ilani kama hizo hazihitajiki na wala si za kirafiki na
hazisaidii katika kupambana na ugaidi wa kimataifa.
Alisema Kenya haitawaachia magaidi kuwatia khofu watu wa Kenya.
0 maoni:
Post a Comment