Takriban wachimba migodi 80,000 wa dhahabu
nchini Afrika Kusini wanatarajiwa kuanza mgomo kudai nyongeza ya mishahara.
Chama cha kitaifa cha
wafanyakazi wa migodini kinataka waongezwe mishahara kwa asilimia sitini.
Wafanyakazi hao wiki
jana walikataa pendekezo walilopewa la nyongeza ya asilimia 6 ambacho ni
kiwango cha mfumuko wa bei kwa sasa.
Sekta ya madini ya
dhahabu ndio moja ya sekta kubwa duniani lakini imekuwa ikikumbwa na misukosuko
katika miaka ya hivi karibuni huku ile ya madini ya platinum ikijikwamua
kutokana na athari za migomo iliyokumba sekta hiyo mwaka jana.
Inakisiwa kuwa migomo
hiyo ya wachimbaji migodi ikiwa itafanyika, itapotezea nchi hiyo zaidi ya dola
milioni 30 kila siku.
0 maoni:
Post a Comment