Taarifa kutoka mjini Mombasa pwani ya Kenya zinasema kuwa vijana
wameteketeza kanisa katikaghasia ambzo zimezuka kufutioa kuuwa kwa muhuburi wa
kiisilamu. Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa keenye ghasia hizo.
Sheikh Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na
washirika wake watatu.
Polisi wamesema kuwa muhubiri huyo alikuwa amehubiri katika
msikiti uliohusishwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab.
Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku wa kuamkia leo
huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa waisilamu na maafisa wa
usalama mjini humo.
Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika msikiti alipokuwa
akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi.
Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa wanarejea nyumbani Alhamisi usiku
baada ya kuhubiri.
Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali
yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama Al Shabaab.
Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka
jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo.
Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi
lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa
Kundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo
ya kigaidi.
Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la
al-Shabab na baadhi ya waisilamu
walioshutumu polisi waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu
wala.
Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo,
alipohutubu katika msikiti huo.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment