Kenya imetoa majina ya wanaume wane ambao inasema
walifanya shambulio dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi majuma
mawili yaliyopita ambapo watu zaidi ya 60 waliuwawa.
Wanaume
hao walionekana kwenye picha za kamera za usalama zilizopatikana Westgate baada
ya jumba hilo kuvamiwa kwa siku nne.
Msemaji
wa jeshi aliwataja wanaume hao kuwa Abu Baara al-Sudani, Omar Nabhan, Khattab
al-Kene na Umayr.
Hakuna
maelezo zaidi yaliyotolewa.
Taarifa
mjini Nairobi zinaonesha kuwa wawili kati yao wana uhusiano na al-Qaeda na
mmoja ana uhusiano na kundi la al-Shabaab ambalo lilisema lilishiriki katika
shambulio la Westgate.
Taarifa hii imetoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment