Watu kama 15 wameuwawa kwenye mapambano nchini Misri
wakati wafuasi wa rais wa Kiislamu, Mohammed Morsi, walitumia siku ya kukumbuka
vita dhidi ya Israel vya mwaka wa 1973, kulaani hatua ya jeshi ya kuitoa
madarakani serikali ya rais huyo.
Askari
wa usalama walitumia moshi wa kutoza machozi na kufyatua risasi hewani
kuwazuwia wafuasi wa Morsi kufika medani ya Tahrir mjini Cairo.
Maelfu
ya watu walishiriki Tahrir katika shughuli zilizotayarishwa na jeshi
kuadhimisha siku hiyo.
Ghasia
piya zilizotokea katika maandamano kama hayo kwenye miji kadha mengine ya
Misri.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment