Wanachama wa kundi la al-Shabaab nchini Somalia wanasema kuwa mji wao
kusini mwa Somalia umeshambuliwa na wanajeshi wa mataifa ya Magharibi.
Wapiganaji hao wanasema wanajeshi wazungu waliuvamia mji wa
Barawe usiku wa manane.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema mpiganaji mmoja aliuwawa na
risasi nyingi zilifyatuliwa.
Baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa helikopta ilitumiwa kwenye
shambulio hilo.
Wengine wanaeleza kuwa wanajeshi waliingia usiku wakitokea
pwani.
Kundi la al Shabaab limesema kuwa lilifanya shambulio la mwezi
uliopita mjini Nairobi dhidi ya jumba la maduka ambalo kwa sehemu linamilikiwa
na Muisraili.
Miaka mine iliyopita jeshi la wanamaji wa Marekani liliuvamia
mji wa Barawe kumuuwa mtu aliyeshukiwa kuwa mfuasi wa al-Qaeda.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment