Amina Mohamed,waziri wa mambo ya nje wa Kenya |
Wasiwasi kuwa Tanzania ingejitoa kutoka jumuia ya Afrika Mashariki ulitokana na hali iliyojitokeza kwa baadhi ya nchi za jumuia hiyo kuendesha mikutano yao bila kuishirikisha Tanzania na Burundi.
Baadhi ya wanasiasa na wananchi nchini Tanzania walitaka nchi yao iachane na jumuia hiyo wakizishutumu Kenya, Rwanda na Uganda kuitenga Tanzania hata katika mikutano ya masuala yaliyohitaji maamuzi ya jumuia.
Kufuatia mfarakano huo, ulionekana kutishia uhai wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, wiki hii alilihutubia bunge la Muungano wa
Tanzania mjini Dodoma, katikati ya nchi na kutangaza bayana kuwa Tanzania haitatoka katika jumuiya ya Afrika Mashariki, kwani imefanya kazi kubwa kuifufua na kuiunda upya baada ya kusambaratika mwaka 1977.
0 maoni:
Post a Comment