MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

MAREKANI NA UINGEREZA ZAPELEKA MISAADA UFILIPINO



 
Siku nne baada ya Kimbunga Haiyan kupiga mji wa Tacloban ,Ufilipino, maelfu ya watu wangali wanasubiri msaada wa dharura.

Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa msaada wa dola millioni 301 ili kuwasaidia watu nchini Ufilipino.

Wakitoa ombi hilo mjni Geneva ,wafanyikazi wa umoja huo wamesema maswala yanayopewa kipaumbele ni chakula,maji na dawa licha ya kuwa maeneo mengi bado hayawezi kufikiwa.

Wakati huohuo, Meli za Marekani na Uingereza zinaelekea nchini Ufilipino huku Umoja wa Mataifa ukiomba msaada kupelekwa nchini humo kukiwa na taarifa za uharibifu mkubwa uliosababishwa na kimbunga Haiyan.

Marekani imepeleka ndege na meli za mizigo kwenda Ufilipino, wakati ambapo Uingereza imepeleka meli ya kivita.

Watu wapatao 10,000 wanahofiwa kufa, na maelfu ya walionusurika katika kimbunga Haiyan wanahitaji msaada.

Rais wa Ufilipino Benigno Aquino ametangaza hali hiyo kuwa janga la kitaifa.
Katika taarifa yake, Rais Aquino,amesema majimbo mawili ya Leyte na Samar yameathirika zaidi kutokana na kimbunga hicho, ikiwemo watu wengi kupoteza maisha
 
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment