Mr. Blue |
MR.BLUE , A.K.A Kabayser, anatafutwa na
Polisi wa nchini Kenya kwa
shutuma za kushindwa kufanya show aliyosaini mkataba mjini Mombasa ,Kenya.
Msanii huyo alitakiwa kufanya show kwenye maeneo ya Office Restaurant, Likoni
na Mariakani Jubilant Hotel November 16 na 17 mwaka huu.
Sammy Ondwar Onyango, ambaye ndiye aliyekuwa mratibu
wa show hiyo ameshtaki kwa polisi wa nchini Kenya kwasababu alishampa Mkwanja
nusu kati ya ule waliokubariana wenyewe kufanya show hiyo.
“ Mr Blue, si mwaminifu kabisa aliwahi kuniangusha pia
mwaka 2012 kwenye show ya Jet Bar, Likon baada ya kudai kuwa alikosa basi la ya
kwenda Mombasa na nililazimika kuingia zaidi Mfukoni kumlipia Basi jengine,”
hayo yalikua maneno ya Onyango.
Inadaiwa kuwa alishapewa kiasi cha laki nne {400,000}
kati ya 1.8, walizokubaliana kwa show nzima, MR Blue, alipopigiwa simu alijibu kwa
sms kuwa naendesha Gari, lakini alipopigiwa tena hakupatikana katika simu.
0 maoni:
Post a Comment