Unauzungumziaje umoja wa wasanii wa filamu kuhusisha
wasanii wa Dar bila wasanii wa mikoani?
Miles zetu ndizo zinazotufanya tusishirikiane, lakini
tunaweza kushirikiana kwa njia nyingi mbalimbali, lakini tunatembeleana.
Lakini ukumbuke
kwamba Dar es Salaam ndio kila kitu, kwa hiyo tunaamini kwamba tukifanya kitu
kizuri na wenzetu wa nao watatengeneza. Mwanza
watatengeneza, Arusha watatengeneza.
Lakini hata
Mwanza nao naona wana Club na Arusha pia nimeona. Lakini wanafanya vile kwa
vile wameiona Bongo Movie Club, lakini vilevile wote tuko chini ya TAF.
Hatujawahi kukataa wasanii wa mikoani kuingia Bongo
Movie, mimi kama Mwenyekiti wa mipango nasema
tunawakaribisha.
Inasemekana wasanii wa filamu walisusia mualiko wa
bunge wakati wa mjadala wa muswada wa sheria ya filamu, kwa nini mlisusia
mualiko muhimu kama huo?
Unajua bahati mbaya au nzuri nyie ndugu zetu
mnachelewa kupata hizi taarifa. Haiwezekani leo mimi nikupe wewe mwaliko
nikwambie kesho njoo Dodoma.
Lazima uniandae
jamani, usiamini mimi kila siku tu nina fedha, sisi ni wasanii tunaprogram ya
muda mrefu, tuna mambo ya muda mrefu tumeyaweka kwenye program zetu.
Lakini vilevile sisi katika uongozi tuna viongozi
wakuu wa club, wa chama cha TAF wanaweza kutuwakilisha, ndio kazi zao sio
lazima wote twende.
Lakini vilevile katika mualiko huu wa bunge ulikuwa
unaongelea nini? Ulikuwa unaongelea kwamba filamu ambazo zitakuwa zimetoka
katika maadili ya kitanzania zilipe faini ya milioni tano. Kwa kiasi gani cha
fedha tunazolipa hadi sisi tuweze kulipa milioni tano?
Na nikaona baadhi ya wabunge wakatutetea vizuri,
wakasema hawa watu ni kiasi kikubwa sana
tunyamazishe kwanza hizi pirates.
Sisi kama serikali ikitu-back up tukauza vizuri filamu
tukapata faida, wewe huoni ajabu mtu kwa mwaka anatengeneza movie tisa, wewe
huoni hicho ni kitu cha ajabu?
Hamna duniani mtu anatengeneza movie tisa kwa mwaka,
inamaanisha movie moja inatengenezwa wiki moja? Hiyo nini sasa si ni kicheko.!
Lakini anafanya hivyo ili kupata faida.
Kama ungepata nafasi ya kuongea bungeni ungelieleza
nini bunge kuhusu tasnia ya filamu Tanzania?
Ningewaambia waheshimiwa wabunge,mheshimiwa Spika,
naomba kwanza tuthamini mali
zetu. Tumekuwa tukipoteza hata mila na desturi, sasa hivi hata ngoma
hizi..zamani zilikuwa zinathaminiwa.
Naomba ninyi
wabunge mkianza kupenda mali
zenu mkaziongelea hapa na kuzitilia mkazo. Sheria mkabala ikapita ya kwamba mtu
akikamatwa ametoa copy tofauti na TRA, hazina sticker adhabu itatolewa,
aidha miaka 10 jela unadhani nani
angefanya hii biashara. Wasanii wangefaidika.
Lakini inashindikikana kutokana na sheria yenyewe. Kwanza unaambiwa wanaofanya hiyo pirates ni haohao watu
wakubwa. Kwa hiyo ukienda anakwambia..nini, ngoja nimpigie simu mtu fulani.
Inasemekana unapewa msaada mkubwa na mtoto wa rais
ndio sababu huikosoi sana serikali kwa kutumia sauti ya Mwalimu kwenye movie
zako, ni kweli?
Mi nataka kukwambia kwamba Nyerere ana kampuni yake ya
Steve Nyerere The Power, na hapa napoliongelea si ni bunge la Jamhuri ya
muungano wa Tanzania.
Si kuna chama tawala na chama tawala, si ninataka wote watutetee, sasa hapa
nani ninayemtetea?
Sanaa ya Tanzania imeinuka baada ya rais
Kikwete kuonesha dhamira nayo. Sisi tumeheshimika baada ya rais Kikwete
kuonesha dhamira nayo na kusema ‘jamani hawa wasanii wa Tanzania lazima
wafaidike’. Lakini pili mimi nimekuwa mtu mwingine tofauti, nimetoa movie ya
Mwalimu Nyerere na ukiangalia ile movie mpaka mwisho nimeongelea matatizo
ambayo Mwalimu alikuwa anayaongelea ambayo mpaka sasa hivi yanatokea.
Juzi nilikuwa nahojiwa kwenye TV flani, nimesema…nchi
hii sasa hivi waziri hajamaliza kazi ya uwaziri, hajamaliza uwakilishi wa jimbo
lake bungeni na anaanza kutangaza anagombania
urais! Ni shida.
Unaizungumziaje kauli ya Dude kuwa ni Kanumba pekee
ndiye aliyekuwa anaitangaza Tanzania kimataifa, lakini wasanii wa sasa hivi
hawafanyi hivyo?
Siku zote aliyekufa anasifiwa, hata jambazi anasifiwa
ndugu yangu. Lakini hata Steve alikuwa ana mipango, alikuwa ana muda mrefu wa
kutaka kujiandaa kutengeneza hivyo vitu. Huwezi tu ukakurupuka leo ukaanza
kumgeza Steve Kanumba eti kwa sababu alikuwa anaitangaza eti na wewe uanze
kutumia hela yako yote ya movie kuzunguka tu halafu ukirudi nothing.
Lakini wapo, kuna watu wanaenda kushoot Kenya,
Monalisa kila siku anaenda Ghana
hapo anaitangaza nchi. Mimi juzi nilikuwa Rwanda…tupo. Kwa maana hiyo sio
kila nikienda Ulaya nijiweke kwenye blogs, nikienda Sweden nijiweke kwenye
mablog, ni mambo ya kizamani, uko sijui chooni nijiweke kwenye Instagram, aah
ni mambo ya kizamani.
Ni movie gani ambayo uliwahi kuuza ukapata pesa nyingi
zaidi, na uliuza shilingi ngapi?
Faida ya movie ya Mwalimu Nyerere ilikuwa milioni 15,
faida ya Mr. President ilikuwa milioni
15 pia. Kwahiyo zote zililingana.
Unajua movie za siasa zinahitaji uhusika kamili, upate
mabenz, ufanye vikao, unahitaji watu wengi na wote unawalipa. Kwa hiyo movie
ukiwa huna milioni 20 hadi 30, na hapo 20 umeibana movie sana kuna vitu vingi
vya msingi umevitoa.
Kwa hiyo nachotaka kusema ifikie hatua movie moja iwe
ina gharimu milioni 100, kwa sababu kuna vitu vingi sana vya msingi vya kuweka
kwenye movie Tanzania.
Lakini mi nimeona kuna msanii mmoja alipewa milioni 10
akatengeneza movie 3, na ni msanii mkubwa nchi hii. Lakini yote hiyo ili apate
faida.
Unayazungumziaje maisha ya King Majuto na mchango wake
kwenye tasnia ya filamu,na je, umeshawahi kuigiza naye ama una mpango?
Bado sijawahi kuigiza naye, lakini natarajia kufanya
nae kazi.
King kaanza kupata hela sasa hivi, ana daladala, ana
magari, ana hela. Watanzania wameanza kujua thamani ya King. Ni sawa sawa
msanii akifa, we ulikuwa unajua Kanumba angejaza watu wote wale? Mungu angempa macho aone dakika tatu tu si
angeona amekuwa Oprah au Jay- Z. Kwahiyo nachotaka kusema watanzania wanajua
thamani ya msanii akifa, tofauti na wenzetu wanajua thamani ya mtu akiwa hai.
Ni wachekeshaji gani watano unaowakubali zaidi
Tanzania?
Marehemu Sharo alikuwa anakuja vizuri kwa sababu
alikuwa mbunifu, mimi napenda mtu mbunifu, na alikuwa ana uwezo mkubwa.
Joti, anabadilika badilika. Ukimuweka kwenye utoto
anaweza, mwanamke anaweza. Ingawa kidogo sasa hivi ku-act ile umevaa vitumbo
imepitwa na wakati. Kwa sababu dunia inaenda na hii mnaiita digitali,
vimebadilika lakini ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa.
Mtu mwingine Mboto, Mboto ana uwezo lakini hajijui
anataka nini. Lakini ni mtu ambaye akikaa akisimama strong ukimwambia cheza
hivi cheza vile, anakuchekesha.
Mtu wa nne ni King Majuto, lakini mtu wa mwisho ni
Kingwendu. Mimi naamini Kingwendu hajapata management sahihi lakini ana uwezo
wa kufanya kitu kizuri.
Unadhani watanzania wanamuenzi Mwalimu Nyerere
Ipasavyo?
Steve: Hatuwezi kumuenzi Nyerere ipasavyo. Wezi
wamekuwa wengi serikalini sasa tunamuenzi vipi? Zamani Nyerere alikuwa na kitu kinaitwa ‘Sisi’. Inamaanisha wewe, mimi
na yule tupate wote. Lakini siku hizi kuna kitu kinaitwa ‘Mimi’, inamaanisha
wewe usipate niwepo mimi tu.
Ndo maana unakuta mtu amestaafu anaongezewa miaka
miwili, na wale waliomaliza chuo kikuu wafanye nini?
Toka miaka miwili nyuma, rais Kikwete alipoanza awamu
yake hii ya pili ni watu wangapi wameshatangaza kugombea urais? Karibia 34. Mpaka
diwani anataka urais, ni aibu. Huko ikulu kuna nini. Lakini enzi za Nyerere
kulikuwa hamna, watu walikuwa wanaheshimu. Ilikuwa angalau bado miezi miwili
ndo mtu unajua anania ya kutaka urais.
Sasa hivi hakuna mkemeaji, sasa hivi kila mtu
anakemea, kila mtu ana hisa. Na tunapoelekea masikini ataendelea kuwa masikini
na tajiri ataendelea kuwa tajiri.
Mkataba wako na Proin Entertainment uko vipi na
unafaidika vipi kusimamiwa kazi zake na Proin?
Kazi zangu zote zinasimamiwa na Proin Entertainment,
na sasa hivi wananitangaza nje ya nchi. Kwa mfano sasa hivi nina show yangu
London ntaenda kufanya. Nimepata bahati ya mualiko mzuri wa kwenda kuhojiwa
BBC, nadhani mwezi wa kwanza Mungu akijalia.
Kwa hiyo hivyo ni vitu ambavyo vitanitangaza mimi kama
Steve Nyerere ninayemuenzi Nyerere. Kwa sababu vizazi vya sasa vimeanza kusahau
mwalimu alikuwa nani. Kwa hiyo mimi ni jukumu langu kuwakumbusha. Ntaendelea kutengeneza movie za mwalimu kwa
mwaka angalau movie moja.
Kutoka Times fm 100.5
0 maoni:
Post a Comment