Steve Nyerere |
Muigizaji wa Bongo Movies, Steve Nyerere,
amefunguka na kusema kuwa maisha ya kifahari wanayoishi wasanii wengi wa kike
sio maisha halisi yatokanayo na kazi za sanaa wanayoifanya.
Aliendelea kusema kupitia 100.5, Times Fm, kuwa watu wasiangalie maisha
ya kifahari yanayooneshwa na baadhi ya wasanii hao kwenye magazeti wakadhani
kuwa yanatokana na filamu wanazozifanya.
Sisi wanaume upande wa Bongo Movies, kupata pesa
tunategemea Movies zetu, lakini dada zetu wana njia nyingi za kujipatia pesa
ambazo sisi wanaume hatuziwezi kuzitumia.
Alikazia kwa kusema kuwa “ watakuja tu watu wametokea
Marekani, wametokea Buzwagi, watakuja watu wametokea wapi kule…wanamtaka dada Fulani,
kwanza hawawezi kuja na kusema 10 hii hapa.. dada zetu ni watu wa Show Shine,
unawajua tena lazima waoshe , anunue Cheni atoe kwenye Gazeti, watu wakiwaona
kwenye magazeti wanajua kuwa ndivyo wanavyoishi, wakati sio hivyo, hayo
yalikuwa maneno ya Steve.
Alisema kuwa hauwezi kumfananisha JB na Wolper au
Wema, hauwezi kumfananisha Steve Nyerere na Shilole, hauwezi kuwafananisha hao
watu kwa kuwa wana njia nyingi, kwa siku anaweza kupigiwa simu 34, mimi kwa
siku nikapigiwa simu moja tu tena na Producer .
Muigizaji huyo amewaomba viongozi wa serikali
kutoangalia pesa, vitu vya kifahari ambavyo vinaandikwa kwenye magazeti au vitu
vinavyonunuliwa na wasanii wa filamu na kuwaza kuwa kuna pesa nyingi
zilizokumbatiwa kwenye tasnia hii, hali
halisi haiku hivyo
0 maoni:
Post a Comment