Wafanyabiashara na wachuuzi waliandaman mjini Mombasa kupinga kutozwa kodi na serikali ya jimbo hilo |
Mamia ya wakenya Jumanne waliandamana katika sehemu mbali mbali nchini
humo kupinga kutozwa kodi ya ziada na serikali za majimbo katika juhudi za
kukusanya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Wengi wanasema kuwa Magavana ambao ni wakuu wa majimbo wamekosa ujanja wa kutafuta njia za kupata pesa za maendeleo na kuamua sasa kuanza kuwatoza watu wengi masikini kodi wanazosema hazistahili kutozwa.
Magavana katika baadhi ya majimbo wanawatoza kodi wafugaji wa Ng'ombe,Kuku na hata kutozwa kodi ya kufanya maziko katika sehemu za umma.
Jjimbo la (Kakamega) Magharibi mwa Kenya limeafikia kuwatoza watu kodi kwa kufuga Kuku kwa kila Kuku jambo ambalo limewaudhi wenyeji katika jimbo hilo linalosifika kwa kutumia Kuku kama kitoweo kuliko jamii nyingine yoyote Kenya.
Swala hili limewakera wakenya wengi ambao tayari wanalalamika kutozwa kiwango kikubwa cha kodi na serikali kuu.
Baadhi ya wanasiasa wanataka pawepo sheria itakayozuia magavana kuwatoza kodi za ajabu na kiholela wanananchi wa majimboni ambao kipato chao ni cha chini mno.
Hizi ni baadhi ya changamoto zinazokabili mfumo huu mpya wa utawala wa majimbo nchini Kenya ambao ulikuja kwa katiba mpya mwaka 2010. Kila Jimbo linastahili kujitafutia ushuru ili kufanya miradi ya kuendedeza maisha ya wananchi.
Mbali na hilo majimbo hayo pia yanapewa pesa zaidi za maendeleo na serikali kuu.
Lakini kwa kukosa ujanja magavana wameamua kwenda mifukoni mwa walalahoi kuwatoza kodi ambazo zamani walikuwa hawatozwi.
Mmoja wa wanasiasa wa baraza na Senate Bony Khalwale, antarajiwa kuwasilisha miswaada minne katika baraza hilo kukomesaha magavana kuwatoza wananchi kodi za kufuga Kuku, Mbuzi na hata kuwazika wafu.
Pia anataka sheria itakayozuia magavana kuwatoza kiwango cha juu cha kodi wafanyabiashara.
<BBC><.........
0 maoni:
Post a Comment