MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUFANYIKA ZANZIBAR FEBRUARY 13-16 WASANII ZAIDI YA 200, KUTUMBUIZA SIKU HIYO.



  Tamasha la Sauti za Busara kufanyika Zanzibar February 13-16, wasanii zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali duniani kuhudhuria
Tamasha kubwa la muziki linalosherehekea muziki wa kiafrika kila mwaka ‘Sauti za Busara’, litafanyika February 13 hadi February 16 mwaka huu, Ngome Kongwe Zanzibar na kuhudhuriwa na waasanii 200 kutoka katika nchi za Afrika na wasanii wengine kutoka nchi zilizo nje ya bara la Afrika.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaji wa tamasha hilo (Busara Promotions), linalodhaminiwa pia na 100.5 Times Fm, wasanii hao 200 kutoka kwenye vikundi 32 watafanya maeonesho jukwaani ambapo kila kikundi kitaimba Live kwa kutumia vyombo vya muziki kwa asilimia 100.

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania, Jhikoman anayefanya muziki wa reggae anatariwa kuzindua ziara yake ya kuitembelea dunia, atakapopanda jukwaani wakati wa onesho la Sauti za Busara. Wasanii wengine watakaoutumbuiza kutoka Tanzania ni Ashimba, Swahili Vibes, Hoko Horo, Seven survivor, Abantu Mandingo, Segere Original, na Kazimoto anayemshirikisha Jackie Kazimoto from the Internationally- acclaimed Jagwa Music.

Mwanamuziki mkongwe kutoka Ghana Ebo Taylor pia atahudhuria katika tamasha hilo, na kutoka Gambia mwanamke maarufu katika ulimwengu wa muziki Jobarteh. Jupiter and Okwess International, moja kati ya wanamuziki wenye mafanikio makubwa kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo atazikonga nyoyo za mashabiki wa muziki mzuri.

Katika tamasha hilo mwaka huu kutakuwa na kongamano la wataalam na filamu ndefu za muziki wa kiafrika zilizoshinda tuzo mbalimbali zitaoneshwa.
Tamasha la mwaka huu litakuwa na kitu kipya kabisa, wachezea santuri (DJs) watapata nafasi ya kupata mafunzo maalum kupitia mradi unaojulikana kama ‘Santuri Safari’. Mafunzo hayo yatalenga katika kuangalia jukumu la DJ kwa wakati huu na jinsi ya kukuza muziki wa Afrika Mashariki kwa kutumia utamaduni wa DJ.
 Kutoka Timesfm.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment