MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

WAFADHILA WAKATA MISAADA UGANDA.



 
Wafadhili wameanza kuikatia misaada Uganda baada ya Rais Yoweri Museveni kuutia sahihi muswada dhidi ya mapenzi ya jinsi moja Jumatatu iliopita.......


Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.
Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.

Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.

Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.

Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.
Kutoka BBC.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment