Mpango wa pamoja kukabiliana na utumwa mamboleo pamoja na biashara
haramu ya binadamu umezinduliwa na Kanisa Katoliki, Kanisa la kianglikana na
Uongozi wa Waislam wa Ki-sunni ambao kiongozi wake ni Imamu wa chuo kikuu cha
al Azhar............
Mpango huo wa Global Freedom Network umezinduliwa Vatican na unanuia kupambana na utumwa kwa kuhimiza serikali, makundi ya wafanyibiashara, waumini na wasomi kumaliza mitandao ya utumwa.
Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu millioni thelathini wamezuiliwa kote duniani na kulazimishwa kuwa wafanyikazi wa nyumbani, watumwa wa ngono, watoto wanaotumiwa kama wanajeshi na wafanya kazi nyingine za mikono.
Mpango huu utashirikiana na kikundi cha wanaharakati cha Free Foundation.
0 maoni:
Post a Comment