Wakali wa soka Duniani, Real Madrid, imechezea kichapo
cha mabao mawili kwa moja katika mchezo uliochezwa hapo jana usiku,.................
Real Madrid
ambao walikua wanapewa nafasi kubwa ya kurejesha ubingwa wa ligi ya nchini
Hispania mbao kwa sasa unashikiliwa na FC Barcelona, walijikuta wakipoteza
mchezo huo, baada ya kuzidiwa maarifa na wenyeji wao ambao walipata mabao ya
ushindi kupitia kwa Carlos Bacca alifunga katika dakika ya 19 na 72
Kwa upande wa kikosi cha Real Madrid, kilipata Bao la
kufutia machozi la Real Madrid
lilifungwa na Cristiano Ronaldo katika dakika ya 14 ya mchezo huo.
Jana hiyo hiyo vijana wa Atletico Madrid ambao pia usiku wa kuamkia hii
leo walikua uwanjani, wameendelea kukaa kileleni kufuatia ushindi wa bao moja
kwa bila lililofungwa na mshambuliaji Diego Costa katika mchezo uliowakutanisha
na Granada CF.
0 maoni:
Post a Comment