Nyumba ya Zuma, kwa muonekano mpya |
Ripoti iliyosubiriwa kwa hamu kuhusu ufisadi nchini Afrika Kusini,
imemkosoa vikali Rais Jacob Zuma kwa kujinufaisha na pesa zilizotumiwa
kuikarabati nyumba yake binfasi katika mkoa wa Kwazulu Natal...............
Ukarabati huo uligharibu dola milioni 23.
Katika ripoti yake , mdhibiti wa mali ya umma nchini humo,Thuli Madonsela, amesema kuwa Zuma alikiuka sheria za maadili na kujifaidisha na pesa za Umma.
Inaarifiwa Zuma alisisitiza ukarabati huo, ufanywe.
Hata hivyo, ripoti hiyo ilisema kuwa hakudanganya wabunge kuhusu kashfa hiyo. Kadhalika wito umetolewa kuwa Zuma arejeshe sehemu ya pesa hizo ambazo hazikutumika kwa ajili ya usalama wake au vinginevyo.
Vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa baadhi ya pesa za umma zilitumiwa katika kufadhili mahitaji ya kifahari ya bwana Zuma kama bwawa la kuogelea na chumba cha sinema.
Ilivyokuwa nyumba ya Zuma kabla ya kukarabatiwa
|
0 maoni:
Post a Comment