Wapiga mbizi wanaowatafuta manusura katika mabaki ya ferry ya korea
kusini iliozama siku ya jumatano wamefanikiwa kupata miili 13 zaidi,na
hivyobasi kufikisha idadi ya watu 46 waliokufa maji.........
Walifanikiwa kuingia ndani ya ferry hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuvunja dirisha moja la chumba kimoja.
Zaidi ya watu 250 wametoweka,wengi wao wakiwa watoto.
Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa inaathiiri shughuli ya usakaji.
Familia za waathiriwa wa mkasa huo zilizokuwa zikiandamana zilikabiliana na maafisa wa polisi katika daraja moja.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa wakati wa ajali hiyo kulikuwa na nahodha mwengine asiye na uzoefu.
Nahodha huyo alikamatwa pamoja na nahodha wa ferry hiyo na wafanyikazi wengine.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment