Watu kadhaa wameuawa wakati wa jaribio la wizi wa
Ng'ombe katika jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini..............
Afisa mmoja katika eneo hilo Paul Dhel Gum ameviambia vyombo vya
habari kwamba takriban watu 28 wameuawa.
Amesema kuwa polisi wamewaua wavamizi wengi.
Uvamizi huo ulitekelezwa katika eneo la mashambani la
jimbo la Warrap siku ya alhamisi ,na kwamba hakuna maelelzo zaidi.
Haijulikani iwapo mauaji hayo yanashirikishwa na vita
vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali ya Sudan kusini na waasi walio watiifu
kwa aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment