MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

AZAM FC, KUSHIRIKI MICHUANO YA CECAFA, SUDAN, TAARIFA KAMILI HII HAPA.



 
AZAM FC itashiriki michuano mipya ya klabu inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) iwapo tu itasogezwa mbele........


Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’ amesema kwamba wamepata mwaliko wa CECAFA kuombwa kushiriki michuano hiyo ya Mei mwaka huu, lakini wametoa jibu kwa muda uliopangwa, hawataweza.

“Tumewasiliana na CECAFA baada ya kutuomba tutume orodha ya watakaokwenda Sudan, na tumewaambia wazi kwamba muda ambao michuano imepangwa kufanyika, hatutaweza, ila kama watasogeza mbele, tunaweza kujipanga na kwenda,”alisema Father.

Father alisema kwa sasa wachezaji wa Azam FC wapo likizo hadi Juni 15 baada ya kumaliza msimu vizuri na ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakati michuano hiyo mipya itakayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA au washindi wa 
 pili wa Ligi Kuu itafanyika nchini Sudan kuanzia Mei 20 hadi Juni 5.
 
Azam imemaliza Ligi Kuu na pointi 62 dhidi ya 56 za waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC na kuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo

IMG_3174
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment