Kikosi cha Azam Fc, kimeanza kusakam Vipaji vya
kujiunga na akademi ya Azam FC ambayo hufanyika kila tarehe ya mwanzo ya mwezi,
hayatakuwepo kwa miezi ya Mei na Juni, mwaka huu..........
Kocha Mkuu wa Azam Academy, Vivek Nagul raia wa India
amesema majaribio yafuatayo yatafanyika Julai 1 mwaka huu kuanzia Saa 12.30
asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar
es Salaam.
Vivek ameomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
na amewataka vijana wenye ndoto za kujiunga na akademi hiyo kujitokeza Julai 1
kujaribu bahati yao.
“Wazazi pia, ambao wana ndoto za kuwaleta vijana wao hapa, tunapenda kuwaambia
nafasi nyingine kwao ni Julai 1, wanakaribishwa,”alisema.
Taarifa kutoka Azam Fc.
0 maoni:
Post a Comment