Viongozi wa nchi Saba tajiri kwa viwanda duniani G7
wamekubaliana kuongeza vikwazo zaidi kwa Urusi ambapo wamesema imezidi kuifanya
Ukraine
isitawalike.......
Ikulu ya White House ya Marekani imesema wataanza
kuweka vikwazo hivyo haraka iwezekanavyo kuanzia siku ya jumatatu na
wanatarajia kulenga biashara za binafsi na ambazo zina uhusiano na Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Viongozi hao wa G7 wameelezea kuguswa kwa na jinsi
Urusi ilivyoshindwa kuacha kuwasaidia wanaoipinga serikali.
Wametoa wito kwa Urusi kuacha mipango yake kijeshi ya
siri kwenye mpaka na Ukraine.
Kwa upande mwingine viongozi hao wa nchi saba tajiri
duniani wameisifu Ukraine
kwa jinsi walivyojizuia kwa kupanda na wapiganaji waasi.
Serikali ya Ukraine imesema inahofia kuwa Urusi
ina mipango ya kuivamia. Hata hivyo Urusi imesema nchi za magharibi zina
mipango ya kuteka kuitawala nchi yao.
0 maoni:
Post a Comment