MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

HALI YA TAHARUKI YATANDA BANGUI



Wanajeshi wanashambuliwa na wapiganaji wa kikrsito wa Anti Balaka

 Umoja wa Mataifa unasema hali ya usalama katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati imeendelea kuzorota, huku taharuki ikiendelea kutanda kati ya walinda amani na wapiganaji wa kikristo Anti -Balaka...............


Taarifa zinasema kwamba zaidi ya watu 20 waliuawa na 100 kujeruhiwa hapo Jumamosi wakati wanajeshi wa Chad walipowafyatulia risasi wakaazi wengi ambao ni Wakristo.

Mmoja wa majeruhi Matilde Ewaton ameambia BBC kuwa wakaazi wengi wa Bangui walikimbilia usalama wao wakati wanajeshi wa Chad walipoanza kuwafyatulia risasi na kurusha makombora.

Shirika la Umoja huo la kuwahudumia wakimbizi, limesema kuwa karibu watu elfu kumi na sita wameachwa bila makao katika siku kumi zilizopita.
Wengi wametoroka vita vinanyoendelea kupamba moto mjini Bnagui ambako watu sitini wameuawa hivi maajuzi.

Zaidi ya watu 20 kati ya waliofariki waliuawa na wanajeshi wa Chad waliowafyatulia risasi Jumamosi katika mtaa wenye wakristo wengi.

Kwa mujibu wa Umoja huo, wapiganaji wa kikristo wamezidisha mashambulizi dhidi ya waisilamu na walinda amani wa Muungano wa Afrika.
Kutoka BBC
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment