Madaktari katika hospitali kubwa zaidi ya umma nchini
Kenya,Kenyatta, wamefanikiwa kutoa risasi iliyokuwa imekwama katika ubongo wa
mtoto Satrine Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.................
Risasi hiyo iliyomuingia mtoto Satrine kichwani ndiyo
iliyomuua mamake.
Mamake Satrine alikuwa amempakata mtoto wake ili
kumlinda kutokana na magaidi waliovamia kanisa walimokuwa wiki moja iliyopita
katika mtaa wa Likoni mjini Mombasa.
Lakini walimpiga risasi mama huyo na kumuua papo hapo
huku risasi iliyomuua mama huyo ikiingia kichwani mwa Satrine na kukwama kwenye
ubongo wake.
Satrine alipelekwa Nairobi
kwa matibabu maalum kutoka Mombasa
kutokana na ukosefu wa wataalamu wa upasuaji wa ubongo mjini humo.
Shughuli ya kuondoa risasi hiyo ilichukua saa tatu na
ilifanywa na madaktari watatu wakiongozwa Daktari Mwangi Gichuru ambaye ni mkuu
wa kitengo cha upasuaji wa neva katika hospitali hiyo.
Matoto Satrine yuko salama na daktari Mwangi anasema
hawakupata matatizo walipokuwa wanafanya upasuaji huo.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment