MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

ICE CUBE, AZIPONDA TUZO ZA MTV, NA TUZO YA PAUL WALKER.



 Ice Cube aziponda
Ice Cube, amefunguka na kuziponda Tuzo za MTV, kwa kumpa marehemu Paul Walker, na Vin Diesel, tuzo za “Best Onscreen Duo” ............


Ice Cube ameliambia gazeti la USA Today kuwa Paul Walker alipewa tuzo hiyo kwa sababu tu ya huruma na sio vinginevyo lakini tuzo hiyo alistahili kupewa yeye na Kevin Hart kupitia comedy yao ya ‘Ride Along’.

Aliendelea kwa kusema kuwa “Aibu yenu, MTV.” Alisema Ice Cube. “Tulikuwa na chemistry bora zaidi kuliko wote waliokuwa nominated, sisi kutoshinda ilikuwa ajabu. Tulikuwa ‘The Best Onscreen Duo’.

Pia aliweka sawa kauli yake kwa kusema kuwa “Walipaswa kumpa kabla hajafariki” .

Rapper huyo alieleza kutofurahishwa kabisa na jinsi ambavyo tukio la utoaji tuzo lilivyoendeshwa kiasi cha kuondoka kabla ya show kuisha.

“Sikuwa nafurahishwa. Nimekuwa nikiingia ndani na nje ya vitu kama hivi kwa miaka 25. Kama haufurahishwi, kwa nini ujitese. Punde unapoona zinakuboa, amka na ondoka.”
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment