Timu ya Mtibwa Sugar, wamefunguka na kusema
kuwa kikosi chao kilikumbwa na changamoto nyiongi sana katika msimu huu
uliokwisha na haya yalikua maneno ya Ofisa Habari wa Timu hiyo........
“Sisi ni wakongwe katika ligi hii, lakini
tumeshindwa kuonesha cheche kutokana na kuwepo kwa timu zenye kiwango kizuri.
Mbeya City fc wametikisa kweli, sio kwetu tu hata Simba na Yanga wamekumbana na
upinzani na ndio maana wamekosa ubingwa ”.
“Kikubwa tumebaini changamoto zetu ikiwemo
kukosa wachezaji muhimu kikosini. Tunataka kufanya usajili mzuri ili tuanze
maandalizi ya mapema”.
“Kufikia mwezi juni lazima mchakato wa
mazoezi utaanza. Tumechoshwa na kuboronga isivyo kawaida yetu”.
0 maoni:
Post a Comment