MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

TATTO YAMTIA MASHAKANI MTALII

Mtalii mmoja muingereza amekataliwa kuingia nchini Sri Lanka baada ya kupatikana akiwa amechorwa 'Tattoo' ya Budhaa kwenye mkono wake.........


Naomi Michelle Coleman, alikamatwa na maafisa wakuu alipowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Colombo baada ya maafisa wakuu kuiona 'Tattoo' hiyo kwenye mkono wake wa kulia.

Budhaa alikuwa mtu mwenye busara na hekima kubwa na pia mwanzilishi wa dini hiyo ambayo mafunzo yake mengi yalijenga msingi wa dini yenyewe.
Msemaji wa polisi alisema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa kwa kosa la kuwachukiza watu wa dini ya Budhaa na pia kwa kuumiza hisia zao za kidini.

Hakimu aliamuru Bi Coleman arejeshwe nchini mwao.

Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao.
Maafisa huchukua hatua kali dhidi ya watu wanaonekana kutusi dini ya Budhaa ambayo waumini wake wengi wanatoka kabila la Sinhalese lenye idadi kubwa ya watu nchini humo.

Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment