MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

AFIA KABURINI WAKATI AKIWA KWENYE JARIBIO LA KUTAKA KUIBA FUVU. PICHA HII HAPA.



 Afia kaburini baada ya kunaswa na kitu akijaribu kufukua ili aibe fuvu
Kijana mmoja huko nchini Nigeria  akutwa amefia kaburini kijana huyo alikubwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina............


Kwa mujibu wa Saturday Tribune la Nigeria, tukio hilo limetokea katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo kwa lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi wakakimbia na kumuacha huku wao wakiwa salama.

“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi na kichwa chake kilikuwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hili waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment