MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

MAELFU WAPINGA KOMBE LA DUNIA BRAZIL



Polisi wa kupambana na ghasia wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya maelfu ya waandamanaji katika barabara za miji ya Sao Paolo na Rio de Janeiro walipinga mfumuko wa gharama ya uenyeji wa kombe la dunia litakaloanza mwezi ujao nchini Brazil...........


Baadhi ya waandamanji walipura mawe na kuchoma magurudumu ya magari na kufunga mabarabara ya miji wakidai serikali haikuzingatia matakwa ya wananchi kama vile elimu sekta ya afya na muundo msingi .

Katika tukio linaloibua hofu ya kuwepo kwa usalama wafanyikazi wa umma na walimu walijiunga na waandamanaji katika miji yote mikuu ikiwemo mji mkuu wa Brasil.

Wengi wao waliahidi kurejea mabarabarani kadri mchuano huo unavyosongea .
 
Mwaka uliopita takriban watu milioni moja walishiriki maandamano wakilalamikia ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na ongezeko la gharama ya uandalizi wa kipute hicho cha fainali ya dimba la dunia .
 

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 12 June.
Waandamanaji walianzia Sao Paulo,karibu na uwanja wa Corinthians Itaquera karibu na mtaa wa Itaquera .

Uwanja huo wa Corithians ndio utakaoandaa mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia mwaka huu tarehe 12 juni.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment