Kichapo walichopatiwa kikosi cha Italy,kilichopelekea
timu hiyo kuyaaga michuano ya kombe la Dunia Huko nchini Brazil,
kumepeleke Timu hiyo kumpoteza kocha wake. Cesar Prandelli..............
Timu ya Italy, imetolewa nje ya michuano hiyo baada ya
kukubali kichapo cha bao 1-0, katika mchezo uliochezwa hapo jana kati ya Italia
na Uruguay,
baada ya kichapo hicho Kocha wa Timu hiyo alikuwa na mkutano na waandishi wa
habari, alitangaza kujiuzulu kuifundisha timu hiyo.
“Nilichagua mfumo fulani wa ukufunzi na ndio sababu
ninajiuzulu, kwa sababu haukufanya kazi,” alisema.
Aliendelea kwa kusema kuwa: “Kuna jambo ambalo
limebadilika tangu nilipotia saini mkataba mpya. Sijui kwanini lakini sina haja
ya kutafuta sababu .”
“Nilizungumza na rais wa shirikisho na naibu wa rais Demetrio Albertini na nikawapa barua ya kujiuzulu kwangu. Ni jambo lisilobadilika,”
0 maoni:
Post a Comment