Baada ya Elizabeth Michael kukana kushirikishwa na
kundi la mapacha kwenye wimbo wao mpya ‘Time For The Money’. Kundi la Mapacha
limeeleza jinsi lilivyoipokea taarifa hiyo...........
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Kulwa wa Mapacha
amesema kitendo alichokifanya Lulu ni dharau kubwa kwao na kwamba inawezekana
ameona hataki kusikika kwenye wimbo waliofanya wao.
“Sisi tuliamua kumtaja kwa respect kwa kuwa tulipenda
alichofanya kwenye ile beat ambayo sisi tuliamua kuiimbia kwa kutumia chorus
yake. Lakini yeye ameamua kutu-disrespect. Sasa sisi tumeamua hata kama wimbo huo ukipata tuzo basi yeye
hatutamtaja...ametudharau.”Alisema Kulwa.
Aliongeza kuwa hivi sasa wameamua kulifuta jina la
Lulu na kwamba hata wimbo huo utakapokuwa unapigwa asitajwe kabisa.
“Sasa hivi tunasimama kama
Magenge peke yetu. Tumeachana na masuala ya Lulu, hatutamtaja
na tunafuta jina lake kabisa
sasa hivi tunabaki Magenge tu.”
Tulipomuuliza kwa nini hawakuwasiliana nae awali
angalau kumshukuru kwa chorus aliyowafanyia ili wapate mrejesho mapema. Alisema
wao hawajawahi kuonana nae wala kuwasiliana nae hata siku moja.
“Tungewasiliana nae vipi, si unajua hawa watoto
unaweza kuwapigia simu wakaacha hata kupokea..si unajua mwanangu. Sisi
tungempata wapi sasa. Tud yeye alituambia ni Lulu na sauti yake kweli ni yeye.
Sasa kama anakataa bana tunaachana nae."
Baada ya Mapacha kutambulisha wimbo wao na taarifa
kumfikia Lulu leo, aliandika kwenye Instagram kwa mshangao mkubwa.
“Mwe mwe mwe...!Mbona mnaninyasanyasa...'in Senga's
voice'
I swear sina
idea na Huku kushirikishwa....au kuna Elizabeth Michael'Lulu' mwingine!????
Dah...hebu
mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn.”
Chanzo Timesfm.
0 maoni:
Post a Comment