Watu wawili wamepoteza maisha baada ya kuporomokewa na Daraja ya juu
mjini Belo Horizonte nchini Brazil.........
Daraja hilo lililokua kwenye ujenzi liliangukia magari yaliyokuwa kwenye foleni chini ya Daraja hilo.
Mji huo ulio kusini mashariki mwa Brazil unatarajiwa kuhodhi michuano ya nusu fainali ya Kombe la dunia juma lijalo.
Idara ya Afya nchini humo imesema kuwa waliopoteza maisha ni dereva wa basi ambalo liliangukiwa na daraja hilo na mtu mwingine mmoja, hali kadhalika watu 22 wamejeruhiwa.
Mamlaka zimesema hawajalifikia gari moja ya abiria ambalo pia liliangukiwa na daraja hilo na haijafahamika kama kulikua na mtu ndani ya gari hilo lakini wamesema watafanya kazi usiku mzima kujaribu kulinasua.
Rais wa Brazil,Dilma Rousseff ameonesha masikitiko yake kwenye ukurasa wake wa Twitter kutokana na ajali hiyo.
Kampuni ya ujenzi iliyokuwa ikijenga barabara hiyo ya juu imepeleka jopo lake la wataalam kwa ajili ya kufanya uchunguzi.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment