Kuna taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayehisiwa kuwa na
virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania...................
Chanzo BBC
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya
Afya ya Tanzania Nsachris Mwamaja mtu huyo ana asili ya Afrika Magharibi ambaye
ni mkazi wa mji wa Dar es Salaam ambaye alifika katika hosptali moja akiwa na
homa kali ikiwa ni dalili mojawapo ya ugojwa huo .
Bwana Mwamaja amesema mgonjwa huyo ambaye ni mtoto wa makamo
tayari ameshatengwa na yupo chini ya uangalizi wa karibu madaktari katika
hosptali Temeke ambayo ni ndio iliyotengwa kwa ajili ya watakaohisiwa kuwa na
ugonjwa huo.
Amesema sababu nyingine ya kuhisiwa kwa mtu huyo kuwa huenda
ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo ni kwa vile hivi karibuni alitokea nchini
Benin.
Hii ni mara ya kwanza ya kuwepo kwa taarifa za mtu kuhisiwa
kuwa na virusi vya Ebola nchini Tanzania.
Taarifa hizi zinakuja baada ya hapo awali serikali ya nchi
hiyo kukanusha taarifa iliyotolewa na gazeti moja la udaku kuwa kuna mgonjwa
mmoja wa Ebola aliyegundulika nchini Tanzania.
0 maoni:
Post a Comment