MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

TAARIFA ZA UGONJWA EBOLA ZALETA MASHAKA KWA WATANZANIA, WIZARA YA AFYA YATOA TAARIFA HII.



Ebola_Virus_Victim
Taarifa kutoka Wizara Ya Afya kuhusiana na uvumi wa Ugonjwa Wa Ebola kuingia nchini Tanzania, ambao kwa sasa unatikisa sana katika nchi NYINGI ZA Afrika,lakini hii ndio Taarifa kamili…………….


Waziri wa Afya wa Tanzania Seif Rashid amesema kuwa wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni wa kutoka Benin na Mtanzania,lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.

Waziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo,Kauli hiyo imekuja baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa kuwa na ugonjwa huo.

Vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa, vimewekwa pia,Wizara ya Afya pia imeongeza uwezo wa kufanya uchunguzi,katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.

Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment