MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

VITA VYAZUKA SUDANI KUSINI.



 
Vita vikali vimezuka nchini Sudan Kusini ,siku chache tu baada ya umoja wa mataifa kuonya kuwawekea vikwazo viongozi wa pande husika kuhusu mzozo huo...............


Mapigano hayo mapya yamesababisha zaidi ya raia elfu arobaini pamoja na wafanyikazi wa misaada kukimbilia hifadhi katika kambi moja ya umoja wa mataifa mjini bentiu.

Idadi ya watu nchini Sudan Kusini tayari inatishiwa kuangamizwa na uhaba wa chakula kutokana na mzozo huo.

Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ambao ulikutana na rais Salva Kiir mbali na kuzungumza na kiongozi wa waasi Riek Machar ,umewataka viongozi hao kuweka kando tofauti zao kwa lengo la kuweka amani.

Zaidi ya watu millioni moja wameyatoroka makaazi yao tangu mwezi Disemba mwaka uliopita
kutoka BBC.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment