Msemaji wa jeshi amewaambia waandishi
wa habari mjini Ouagadougou kuwa bwana Compaore hayuko mamlakani tena...................
Rais Compaore alikuwa ametangaza kuwa
atajiuzulu baada ya kipindi cha serikali ya mpwito ya mwaka mmoja .
Lakini wanasiasa wa upinzani
wakakataa kata kat kuendelea kwa utawala wake na wakamtaka ajiuzulu maramoja.
Rais Compaore alikuwa ameongoza kwa
zaidi ya miaka 27 tayari.
Kumeripotiwa maandamano mapya nchini
Burkina Faso ya kutaka kujiuzulu mara moja kwa rais wa nchi hiyo Blaise
Compaore............
Viongozi wa upinzani wanakutana
kwenye mkji mkuu Ouagadougou kukubaliana kwa pamoja hatua watakazochukua.
Siku ya Alhamisi waandanamaji
walikarisishwa na jitihada za rais za kuongeza kipindi chake chake miaka 27
madarakani na wakateketeza bunge na kusaka kituo cha runinga cha serikali.
Bwana Compaore alitupilia mbali
jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine
kama rais lakini akasema kuwa atabaki madarakani kwa mwaka moja zaidi .
<span >Viongozi wa Upinzani
Nchini Burkina Faso wamewaomba waandamanaji kutolegeza kamba bali kuendelea na
maandamano huku wakimtaka Rais Blaise Campaore ang'atuke mamlakani mara moja.
Licha ya Rais Compaore wa Burkina
Faso kuhutubia taifa siku moja baada ya vurugu kubwa na kutangaza kuvunja
serikali waandamanaji hawataki kusikia kwamba apewe muda wa mwaka mmoja ndipo
aondoke madarakani.
<span >Jana jioni kiongozi wa
Jeshi J<span >eneral Honore Traore alitangaza kuundwa kwa serikali ya
mpwito itakayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja japo hakusema ninani
atakayeiongoza.
Chanzo
BBC
0 maoni:
Post a Comment