Wanasayansi
wamepongeza matokeo ya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, na kusema
dawa zinaonesha kuwa salama na itasaidia mfumo wa kinga ya mwili kuvitambua
virusi hivyo..................
Watu
20 waliojitolea kutoka nchini Marekani, walipatiwa kinga maradhi hiyo, ikiwa ni
hatua muhimu ya kujikinga na virusi hivyo vya ugonjwa wa Ebola.
Utafiti
wa chanjo hiyo ya ebola kama huenda ikaokoa maisha wa maelfu walio hatarini
kuambukizwa virusi hivyo. Dr Anton Fauci ni mkuu wa Taasisi ya Marekani ya
magonjwa ya kuambukiza :
"Kwa
upande wa usalama na uwezo wa kuleta matokeo mazuri nadhani tunaweza kuita
majaribio haya ya chanjo haikufanikiwa. Japokuwa katika mkondo wa awali
imeonyesha mafanikio makubwa." Amesema Fauci
Hata
hivyo watafiti wanasema matokeo hayo sio uthibisho kwamba chanjo hiyo inafanya
kazi lakini kama majaribio ya awali yamekuwa na mafanikio basi chanjo ya eboal
itatolewa kwa maelfu ya wafanyakazi wa afya huko Afrika Magharibi kuanzia mwezi
Januari mwakani.
Zaidi
ya watu elfu tano mia tano wamefariki kutokana na kuambukizwa virusi vya
ebola.Kwa sasa chanjo imekuwa ikifanyiwa utafiti na kampuni GlaxoSmithKline.
Dr
Colin Brown ni mtaalamu wa magonjwa ambaye amepokea habari za chanjo hiiyo kama
habari njema.
"Kwa
vile suala la usalama limepewa umuhimu tunayo furaha kwamba hakuna madhara
yaliyotokana na chanjo. Ambapo imeonyesha wagonjwa wa awali wapatao 20 wakuwa
na tatizo lolote. Ninadhani tutarajie kuona itasaidia hasa kwa upande wa wafanyakazi
wa afya kujilinda wakiwa kazini. " Alisema Bwana Brown
Chanzo
cha Taarifa ni BBC
0 maoni:
Post a Comment