Watu
wapatao wanne wamekufa kufuatia maporomoko ya ardhi kusini mwa Uswisi na
kaskazini mwa Italia kutokana na mvua kubwa zilizonyesha..................
Wanawake
wawili wamekufa wakati tope zito lilipovunja nyumba karibu na mji wa Lugano
nchini Uswisi.
Katika
mpaka, mstaafu na mjukuu wake wa kike waliuawa wakati maporomoko ya udongo
yalipoifukia nyumba yao.
Mvua
kubwa inatarajiwa kuendelea katika eneo hilo, na nchi zote mbili zimetoa ilani
ya tahadhari.
Viwango
vya maji katika maziwa Lugano na Maggiore, ambavyo vilionekana kuwa chini ,sasa
viko juu kabisa na kutishia usalama.
Maporomoko
ya ardhi Italia
Makazi
na maeneo ya biashara, kama vile shamba karibu na ziwa Maggiore nchini Italia,
yamekatwa mawasiliano kutokana na mafuriko.
Eneo
hilo limepata mvua zaidi katika siku chache kuliko ilivyotarajiwa kawaida
katika mwaka.
Kingo
za mto Ticino zimevunjika karibu na Vigevano kaskazini mwa Italia.
Kaskazini
zaidi, katika mkoa wa Ticino nchini Uswisi, wafanyakazi wa uokoaji walikuwa
wakiwatafuta watu walionusurika Jumapili baada ya matope kuporomoa kilima na
kuharibu jengo.
Serikali
ya Uswisi imesema wanawake wawili wenye umri wa miaka 34 na 38 walipoteza
maisha wakati maporomoko ya udongo yalipokumba jengo moja katika kijiji cha
Davesco-Soragno.
Kutoka BBC
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment